Serikali kupitia Wizara ya Afya imewataka
viongozi wote wanaosimamia utoaji huduma katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa
Dodoma kuhakikisha huduma ya x ray inapatikana ndani ya mwezi mmoja ili kuwasadia wagonjwa
wenye uhitaji wa huduma hiyo .
Naibu waziri wa Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dokta Faustine Ndugulile ametoa kauli hiyo leo
alipofanya ziara ya ukaguzi hospitalini hapo ambapo ameshuhudia
wagonjwa wakikosa huduma ya x ray kwa muda wa wiki tatu sasa.
Amesema kuwa licha ya kuwepo
kwa mashine mpya kwa ajili ya huduma hiyo bado wananchi wamelazimika kukosa
huduma hiyo katika mkoa wote wa Dodoma kutokana na mashine iliyokuwa ikitoa
huduma kuharibika hivyo ni wajibu wa viongozi wote wanaohusika kuhakikisha
wanashughulikia tatizo hilo ili huduma ziendelee.
Aidha amewataka watumishi
wote kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagojwa na kuacha tabia ya kutoa lugha
za matusi kwani zipo taarifa zinazodai kuwepo kwa baadhi ya watumishi wanaotoa
lugha chafu kwa wagonjwa jambo ambalo halikubaliki.
Kwa upande wake mwenyekiti
ya bodi ya usimamizi wa hospitali hiyo Dokta Job Lusinde amesema kuwa licha ya
changamoto hiyo bado ipo changamoto nyingine ya kukosa duka la dawa la
hospitali pamoja na nyumba ya kupumzika kwa upande wa akina mama licha ya
kuhudumia wagonjwa wengi wakiwemo wanaotoka katika mikoa mingine jirani.
NA ALFRED BULAHYA DODOMA FM
Comments
Post a Comment