
Wizara
ya mambo ya ndani ya nchi kupitia idara ya wahamiaji imefanikiwa kukamata Jumla
ya wahamiaji haramu 13,393 katika kipindi cha Mwezi July 2017 hadi March 2018.
Naibu
Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni ameyasema hayo Bungeni
Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mh. Faharia Shomali
aliehoji ni wahamiaji haramu wangapi wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo
vya sheria.
Amesema
wahamiaji haramu 13,393 kati yao wahamiaji 2,815 walishitakiwa, 117 walitozwa
faini, 429 walifungwa, 6316 waliondoshwa Nchini, 1353 waliachiwa huru baada ya
kutoa nyaraka za uthibitisho wa uhamiaji wao na kesi zigine 2363 zinaendelea
katika mahakama mbalimbali Nchini,
Amesema
jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuhakikisha wahamiaji haramu hao
wanarudi Nchini mwao baada ya kumalizika kwa vifungo vyao zoezi ambalo hufanyika
kwa kuratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na taasisi ya uhamiaji Dunia IOM
Baada
ya kukamilika kwa shughuli vikao vya bunge, waziri wa ulinzi na jeshi la
kujenga taifa Dokta Hussen Ally Mwinyi akimuwakilisha waziri mkuu amewaongoza
wabunge katika zoezi la kuuaga mwili wa aliekuwa mbunge wa jimbo la buyungu
wilayani kakonko marehemu Kasuku Samsoni Bilago ambapo amesema tukio hilo
linawakumbusha wanadamu kuishi kwa kutenda mema wawapo duniani.
Mwili
wa aliekuwa mbunge wa jimbo la Buyungu Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Marehemu
Mwl. Kasuku Samson Bilago unatarajiwa kupumzishwa katika makao yake ya milele mapema
hapo kesho Wilayani Kakonko .
Na Pius Jayunga Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment