Wachezaji wa timu ya Yanga wameshauriwa kujituma ili kupata matokeo
katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika ili kupata pesa nyingi
ambazo zitaweza kutatua matatizo yanayo wakabili.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na kusema kwa sasa wachezaji wa Yanga wanapaswa kutuliza akili na kuongeza jitihada katika michuano hiyo.
Mwigulu amesema kuwa anafahamu wachezaji wanadai pesa nyingi kwa klabu lakini kama watafanya vizuri watapata hela nyingi kuliko wanazodai.
"Wachezaji wa Yanga wanapaswa kujitambua na kuelekeza akili katika michuano ya Shirikisho ambako wanaweza kupata kiasi kikubwa cha pesa kuliko wanachoidai klabu," alisema Mwigulu.
"Wachezaji wa Yanga wanapaswa kujitoa sana katika mechi za makundi Afrika kwakua watapata pesa nyingi kwa mustakabali wa maisha yao," alisema Mwigulu.

Comments
Post a Comment