Sheria ya ndoa ya
mwaka 1971 ambayo inaeleza mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 hadi 18
kuolewa kwa ridhaa ya baba au mlezi wake imetajwa kuathiri zaidi watoto ambao
wanaishi katika familia masikini na duni kutokana na kuolewa kwa umri
mdogo.
Akizungumza na
DODOMA FM mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye pia ni mwanasheria kutoka
jijini Dar es Salaam bwana Jebra Kambole amesema kuna haja ya serikali
kuibadilisha sheria hiyo kutokana na kuwa chanzo kisababishi cha ukatili wa
kijinsia.
Amesema kitendo cha
mtoto kuolewa akiwa na umri mdogo kutokana na sheria hiyo inavyoruhusu kuna
athari kubwa kiafya ambapo amebainisha kuongezeka kwa idadi ya wanawake wenye
FISTULA pamoja na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Hivi karibuni chama
cha waandishi wa habari wanawake nchini TAMWA kiliandaa semina kwa vyombo vya
habari mkoani Dodoma lengo ikiwa ni kuwapa ujuzi namna ya kuihamasisha serikali
kufanya marekebisho katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
Kwa mujibu wa
sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaruhusu mwanamke kuolewa akiwa chini ya umri wa
miaka 18. Kifungu cha 17 kinaeleza kwamba mwanamke ambaye hajatimiza miaka 18
anaweza kuolewa kwa idhini ya baba au kama baba amefariki basi mama na ikiwa
wote wamefariki basi idhini hiyo yaweza kutolewa na mlezi wake.
BERNAD FILBERT
DODOMA FM
Comments
Post a Comment