Mkuu wa mkoa wa
Dodoma DR. BINILITH MAHENGE amemsimamisha kazi aliyekuwa Afisa Manunuzi katika
ujenzi wa majengo ya kituo cha Afya yanayoendelea kujengwa katika Tarafa ya Mpwayungu wilaya ya Chamwino mkoani
Dodoma Bw.Ebby Mwakajila Kwa matumizi mabaya ya
pesa za ujenzi huo.
Tukio hilo
limetokea baada ya Mkuu wa mkoa kufanya
ziara katika ujenzi huo wa majengo ya kituo cha Afya ambapo imegundulika kuwepo
kwa upungufu wa fedha kiasi cha Tsh.milioni 3
ambazo zimetumika kinyume na utaratibu na kumtaka mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Chamwino kusimamia pesa hizo kurudi katika kazi yake.
Akizungumzia juu ya
ubadilifu wa pesa hizo mkurugenzi wa wilaya ya Chamwino Bw. Athumani Masasi
amekiri kuwepo kwa uzembe wa aliyekuwa afisa manunuzi wa awali ambapo
alimwondoa katika sekta hiyo kabla ya mkuu wa mkoa kumsimamisha kazi na
kumuweka mwingine hadi uchunguzi utakapomalizika.
Pamoja na hayo
kamati ya ujenzi wa kituo cha Afya Mpwayungu wakiwakilishwa na mjumbe wao
Bw.Amani Samweli Mazengo wamesema kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazowaikabili
ikiwemo kupishana kwa mahesabu kati ya mzabuni na kamati ya ujenzi.
Mbunge wa jimbo la
Mtera Mh.Livingstone Lusinde pamoja na
mkuu wa wilaya ya chamwino Mh.Vumilia Nyamonga wameishukuru serikali ya jamhuri
ya muungano wa Tanzania kwa kutoa pesa kwa ajili ya unjenzi wa vituo vya Afya
mbalimbali nchini.
Na ANIPHA RAMADHANI CHANZO
:DODOMA FM
Comments
Post a Comment