Serikli imesema ina
mkakati wa kuhakikisha kunakuwepo na akiba ya kutosha ya mazao ya chakula
ikiwemo zao la mahindi na baada ya hapo hakutakuwa na kizuizi cha kuuza
mazao hayo nje ya nchi.
Waziri wa mambo ya
nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga ameyasema hayo
leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Temeke
Abdalah Mtolea aliehoji Serikali ina mpango gani kuruhusu uuzwaji wa mazao ya
mahindi nje ya nchi ili kuruhusu wananchi kufaidika na fursa zilizopo katika
soko la Afrika ya Mashariki.
Amesema dhamira ya
Serikali ni kuhakikisha hakuna changamoto ya upungufu wa chakula Nchini na hasa
zao la mahindi na kinachofanyika kwa sasa ni kujengwa maghara ya kuhifadhia
mazao hayo pamoja na kufanya tathimini ya kutosha ili kuona kiwango cha zao la
mahindi kilichopo Nchini iwapo kinatosheleza kisha itaruhusu akiba ya mazao
hayo kuuza nje ya nchi.
Akielezea njia
zinazotumika kutangaza fursa zilizopo katika jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi
Mahiga amesema hakuna njia tofauti ya kuwafikishia wananchi fursa zilizopo
kinyume na zile ambazo zimekuwa zikitumika ikiwemo njia ya Redio, Television,
pamoja na kufanya makongamano katika maeneo ya Vijijini hatua iliyoleta
mafanikio makubwa.
Katika hatua
nyingine Balozi Mahiga amesema tangu kuanzishwa kwa Bunge la Afrika Mashariki
mwezi nov. 2001 hadi sasa jumla ya sheria 78 zimekwisha kutungwa na sheria 20
zimekwisha kuridhiwa na wakuu wa Nchi wanachama wakati sheria zingine zikiwa
katika hatua mbalibali za kuridhiwa na kusainiwa, huku sheria zilizotungwa
zikiwa zimelenga kuimarisha biashara, kukuza uchumi wa Nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Na
Pius Jayunga Bunge/Dodoma FM
Comments
Post a Comment