
Serikali imesema zoezi
la usambazaji wa pembejeo za kilimo linafanywa na sekta binafisi Nchini
yakiwemo makampuni katika kuifikishia jamii hudumu ya pembejeo za kilimo na
jukumu la Serikali ni kuratibu mahitaji, upatikanaji na matumizi yake.
Naibu Waziri wa
kilimo Dr. Merry Mwanjelwa ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Mjini Mh. Sebastian Simon Kapufi aliehoji ni
lini Serikali itahakikisha inasambaza pembejeo kwa wakati na kwa kuzingatia
msimu wa jiografia na maeneo husika.
Amesema pamoja na
majukumu hayo bado Serikali inaendelea kuandaa mifumo ya kuhakikisha pembejeo
za kilimo zinasambazwa na kuwafikia
wakulima wengi kwa bei nafuu zaidi na ili kutekeleza azima hiyo 2017/18
Serikali ilianza kutumia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na kuhakikisha
mbolea hiyo inapatikana na kusambazwa kwa wananchi.
Amesema mfumo huo
umeleta faida kubwa ikiwemo kuongezeka kwa upatikanaji wa pembejeo za kutosha
kutoka tani 277,935 kwa mwaka 2016/17 hadi tani 310,673.7 mwezi april na
kuchangia kupungua kwa bei ya mbolea kati ya asilimia 11 hadi 39.5 ikilinganishwa
na bei ya mbolea hiyo kabla ya mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja.
Aidha amesema
Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji wa mazao na teknolojia ya hali ya juu
lengo kubwa ikiwa ni kuwawezesha wakulima kuendesha kilimo chenye tija na
kufanikisha upatikanaji wa mazao ya kutosha ili kukidhi mahitaji katika soko la
mazao hayo.
NA
PIUS JAYUNGA DODOMA FM
Comments
Post a Comment