Kutokana na tafiti zilizofanywa na wataalamu wa ugonjwa wa kifua kikuu nchini zinaonyesha mtu mwenye maambukizi hayo ana uwezo wa kuzalisha wagonjwa 10 mpaka 15 kwa wiki endapo atachelewa kupatiwa matibabu.
Akizungumza na Dodoma FM mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu jiji la
Dodoma daktari Yassin Nyoni amesema
endapo mtu atabainika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu ni vyema akaenda
hospital mapema ili kuepusha kuongeza idadi ya watu ambao wataambukizwa ugonjwa
huo.
Amesema mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yupo hatarini
kukumbwa na ugonjwa wa kifua kikuu
kutokana na upungufu wa kinga mwilini ambayo inaweza kukabiliana na bacteria
wanaosababisha ugonjwa wa kifua kikuu.
Hata hivyo ameongeza kuwa uvutaji wa sigara ni hatari na kwamba ni chanzo
mojawapo kinachosababisha ugonjwa huo .
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wameitaka serikali ipige marufuku utumiaji
wa sigara ambapo itasaidia kuondoa tatizo hilo kwa namna moja au nyingine.
Na Benard Filbert
Dodoma FM
Comments
Post a Comment