Naibu
waziri ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge, Kazi Ajira na wenye ulemavu Mh. Athony
Peter Mavunde amesema tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa
Nchini kumekuwa na mafanikio mengi ikiwemo kupanuka kwa wigo wa demokrasia ya
vyama vingi vipatavo 19.
Mh.
Mavunde ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge
wa Jimbo la Kiwani Abdalha Haji Ally alietaka kufahamu ni faida zipi pamoja na
changamoto zilizo jitokeza Nchini baada ya miongo miwili na nusu ya kuwepo kwa
mfumo wa vyama vingi.
Amesema
mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa umekuwa na faida pamoja na
changamoto zake ikiwemo ongezeko la uhuru wa kuchagua viongozi wa vyama vya
siasa walio nadi sera zao, kuongeza uwajibikaji kwa Serikali huku changamoto
zilizo jitokeza ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama za kuendesha gharama
za kisiasa katika ngazi mbalimbali za uchaguzi.
Akifafanua
juu ya uendeshaji wa mikutano ya kisiasa Nchini, Mh. Mavunde amesema si kweli
kuwa Serikali imezuia harakati za kisiasa na badala yake umewekwa utaratibu
maalumu wa kuendesha siasa kutokana na sheria mbalimbali za Nchi huku akiweka
wazi sheria ya vyama vya siasa sura 258
imempa mamlaka msajili kuhakikisha anavilea vyama vya siasa na kusaidia vyama hivyo
katika utatuzi wa migogoro.
Katika
hatua nyingine Mh. Mavunde amesema lengo la Serikali ni kuendelea kukuza
demokrasia ndani ya Nchi na makubaliano ya mwaka 2002 ya kuanzisha chuo cha
mafunzo kwa wanasiasa yataendelea kufatiliwa ili kujenga Taifa la watu wenye
uzalendo na nia ya kutumikia watanzania kupitia chuo kitakachokuwa na jukumu la
kuoka wanasiasa.
Na Pius Jayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment