
Takwimu za utelekezaji wa famili zazidi kuongezeka siku hadi siku Jijini Dodoma pamoja na kwamba elimu imeendelea kutolewa katika jamii.
Akizungumza na
Dodoma fm Mkaguzi wa polisi kutoka Dawati la jinsia AFANDE THERESIA MDENDEMI
amesema kwa mwaka huu takwimu za utelekezaji wa familia zimeongezeka kutokana
na wanawake kuwa ni dhaifu kwa upande wa
kutoa ushahidi mahakamani.
Ameongeza kuwa
matukio ya utelekezaji wa familia ni mengi lakini changamoto kubwa ni kutopata ushirikiano wa kutosha kwa upande wa ushahidi ili kuhakikisha wanawafikisha
mahakamani wanaume hao kwa lengo la kupewa adhabu na kuwa fundisho kwa wengine.
Kwa upande wao
baadhi ya wanawake wa Jiji la Dodoma wamebainisha kuwa ni kweli wanaogopa kupeleka ushahidi kwa
vyombo vya dola Kwa kuhofia kutoa maelezo mbele ya mahakama.
Hata hivyo baadhi ya wanaume waliozungumza na Dodoma FM wamekiri kuwa wanatelekeza Familia kutokana na ugumu wa maisha na changamoto nyingine katika familia.
Na,Mindi Joseph DODOMA FM
Comments
Post a Comment