
Lishe duni kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano imetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu
inayopelekea watoto wengi kupatwa na
tatizo la utapiamlo.
Akizungumza na
kituo hiki afisa lishe mkoa wa Dodoma Bi.MARIAM ATHUMANI MWITA amesema watoto
wengi waliolazwa hospitalini wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo ambapo wazazi
wamekuwa wakichangia kutowajali watoto wao kwa kuwapatia lishe bora.
Bi. Mariamu amesema
utapiamlo unaathari kubwa si kwa watoto tu bali unachangia kuzorota kwa uchumi
wa nchi kutokana na matibabu yake kuwa na gharama kubwa hivyo kuwataka wazazi
kuitendea kazi kauli isemayo KINGA NI BORA KULIKO TIBA ili kuokoa maisha ya
watoto pamoja na rasirimali zao.
Amesema dalili za
awali za utapiamlo humfanya mtoto kutokuwa mchangamfu, kula chakula kingi bila
kuongezeka uzito, kuvimba tumbo na miguu pamoja na kulia mara kwa mara.
Kulingana na dalili
hizo wazazi wameshauriwa kuwahi katika vituo vya afya ili kupatiwa vipimo na
kubaini chanzo cha tatizo hilo kutokana na kuwepo kwa vyanzo tofauti vya tatizo la utapiamlo na
miongoni mwa vyanzo hivyo ikiwa ni magonjwa kama kifua kikuu na UKIMWI.
Na kwa upande wa
baadhi ya wazazi wamesema watoto kukataa kula chakula ni moja kati sababu inayochangia watoto kupata utapiamlo
pamoja na hali duni ya maisha ambayo inapelekea wao kukosa chakula cha lishe
kwa watoto hali ambayo inapelekea kuwalisha watoto chakula wanachokula wao.
Sanjari na hayo Bi
Mariamu amesema wazazi wengi wamekuwa hawazingatii uzazi wa mpango hatua ambayo inawafanya
kushidwa kulea watoto wa muda wa miaka miwili na nusu kwa kuwanyonyesha maziwa
ya mama pekee.
Na
ANIPHA RAMADHANI DODOMA FM
Comments
Post a Comment