Kocha wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya Simba itakayopigwa kwenye Uwanja wa Namfua, amesema kuwa lazima walipe kisasi kwa wapinzani wao hao.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Singida United ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Pluijm alisema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwao kulipa kisasi kwa wapinzani wao hao waliowafunga mabao 4-0.
Comments
Post a Comment