Imeelezwa kuwa ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa sababu
zinazopelekea kinamama wajawazito kujifungua watoto njiti kutokana na ugonjwa
huo kuzuia mtoto kupata chakula kama
inavyotakiwa awapo tumboni.
Hayo yamebainishwa na Daktari wa kitengo cha watoto kutoka
Hospitali ya Rufaa Mkoani Dodoma Dr.Halima Kasimu wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya
Sababu zinazopelekea watoto kuzaliwa njiti.
Dokta Halima ameutaja ugonjwa wa kisukari kama moja ya sababu zinazosababisha mtoto kupata shida ya mahitaji muhimu kama chakula kutoka kwa mama
na kumpelekea kutoka kabla ya miezi 9.
Aidha Dokta Halima amebainisha sababu nyingine inayopelekea
mtoto kuzaliwa njiti kuwa ni mama kutokwa na maji kabla ya siku pamoja na mama
kuwa na mapacha.
Hata hivyo amewataka
kinamama wajawazito kuachana na dhana ya kujifungulia majumbani mwao na badala
yake wahudhurie kliniki kama
inavyotakiwa ili kuchunguzwa afya zao mapema ili kusaidia kupunguza kuzaliwa kwa watoto njiti nchini.
Dokta Halima amewataka wazazi watakaopata watoto njiti kuwalea kwa
kuzingatia maelekezo kutoka kwa wataalamu ili wasiwapoteze kutokana na mtoto
huyo kutokidhi baridi na kuhitaji joto la mama pekee.
Na ANIPHA RAMADHANI CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment