Katika kuendelea
kuhamasisha jamii kujenga na kutumia vyoo bora kupitia kampeni ya taifa ya
usafi inayoratibiwa na Wizara ya Afya kaya zisizokuwa na vyoo zimepungua kutoka asilimia 20. 5
mpaka kufikia asilimia 5. 1 nchini.
Akiongea na Dodoma
fm Mratibu wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu ‘usichukulie poa nyumba ni choo’ kutoka Wizara ya Afya Bw. Anyitike Mwakitalima
amesema tangu kuanza kwa kampeni mwaka 2012
wamefanya tafiti na kubaini kaya 20. 5 hazikuwa na vyoo kabisa na
kupitia kampeni ya nyumba ni choo imepungua na kufikia asilimia 5.1 mpaka sasa.
Bw. Anyitike
amesema katika kutekeleza kampeni kumejitokeza changamoto mbalimbali ikiwemo ya
kitamaduni ambapo wapo baadhi ya watu wenye tamaduni ya kutotumia choo kwa kile
wanachodai kuwa ni laana katika familia pamoja na changamoto zinazohusu
mazingira.
Amesema choo bora
ni choo kinachozuia kuenea kwa kinyesi katika mazingira ya binadamu, kuwa na
sakafu inayosafishika kwa maji, kiwe na usiri, ,lango pamoja na paa.
Hata hivyo amewataka viongozi mbalimbali kuwa mfano wa kuigwa na wananchi wao kutokana na
kuwemo na baadhi ya viongozi wa vijiji katika baadhi ya maeneo kutokuwa na vyoo
hali inayopelekea ugumu kwa baadhi ya wananchi kuwa na vyoo vilivyo bora.
Na
Phina Nimrod Dodoma FM
How can I get contact with nyumba ni choo at dodoma?
ReplyDelete