Ukosefu wa
ajira nchini umetajwa kuwa ni sababu
inayopelekea vijana wengi kutokujitegemea na badala yake kuendelea kuishi na
wazazi wao kwa muda mrefu.
Hayo yamebainishwa
na wakili wa kujitegemea mkoani Dodoma Bwana Cristopher Malinga wakati
akizungumza na Dodoma FM ofisini kwake.
Bwana Malinga
amesema kuwa kulingana na sheria za Tanzania hakuna umri sahii wa kijana kutoka
nyumbani na kwenda kujitegemea isipokuwa ni maamuzi binafsi.
Akizungumzia sababu
kubwa ya vijana wengi kuishi na wazazi wao kwa muda mrefu amesema ni kutokana na ukosefu wa ajira hivyo kushindwa kujiamini
katika uendeshaji wa maisha yake binafsi.
Amewataka wananchi
kuacha kutazama umri badala yake waangalie uwezo wa kuendesha maisha kutokana
na kuwa hakuna sheria yoyote ambayo inamtaka kijana kutoka nyumbani baada ya
umri Fulani kwa mujibu wa tamaduni za Kiafrika.
Na
Benard Filbert Dodoma FM
Comments
Post a Comment