
Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
wametakiwa kuifahamu sheria ya UKIMWI ili kuzitambua haki zao za msingi ambazo
mara nyingi zimekuwa zikikiukwa.
Hayo yamebainishwa na Afisa sheria kutoka Tume ya kudhibiti
UKIMWI Tanzania (TACADS) Bwana Miraji Mambo wakati akitoa ufafanuzi wa sheria
ya ukimwi katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma wa ukihusisha Konga za watu wanaoishi na virusi
vya UKIMWI.
Amesema haki nyingi za watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI zimekuwa
zikikiukwa ikiwemo haki za kutibiwa na
haki za kutobaguliwa huku akilitaka jeshi la polisi na mahakama kuifahamu
sheria hiyo ili waweze kutekeleza
matakwa ya sheria hiyo.
Mapema akifungua kikao hicho cha kuzijengea uwezo Konga za watu
wanaoishi na virusi vya Ukimwi, Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
kudhibiti Ukimwi Tanzania TACADS Bwana Jumanne Isango amesema mapambano dhidi
ya Ukimwi ni hatua endelevu katika kuhakikisha watu wanaoishi na virusi vya
Ukimwi wanakuwa kwenye uangalizi na kwamba sheria ya Ukimwi ni muhimu katumika
ili kulinda haki zao.
Ameongeza kuwa ili kufikia malengo ya mwaka 2030 ya kutokuwa na
maambukizi ya ukimwi jamii inatakiwa kushishirikiana katika nyanja zote bila
kubagua jinsia wala kabila.
Mkutano huo wa siku moja umehusisha Konga za watu wanaoishi na
virusi vya ukimwi kutoka halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Dodoma,
Singida,Shinyanga na Tabora wakiwemo wawakilishi wa polisi kutoka iringa ,
Tabora, Dodoma , Singida na Dar es Salaam.
Na
ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment