Katika kuhakikisha
takwimu za wagonjwa na watu waliofariki zinatunzwa kituo cha afya Makole Jijini Dodoma kina mkakati wa
kununua talakilishi 30 zitakazo saidia kuhifadhi takwimu hizo kwa mfumo wa
kidigitali.
Akizungumza na Dodoma FM Mganga Mkuu wa kituo cha afya Makole Dk.George Batiku amesema ukitaka kupata takwimu zote za wagonjwa katika
hospitali kwa urahisi ni muhimu kutumia njia ya kidigitali ukitofautisha na
utumiaji wa karatasi kwa ajili ya uhifadhi wa takwimu.
Dokta George
amesema wameanza kutumia njia mpya za kuhifadhi taarifa kidigitali isipokuwa
wanakabiliwa na changamoto ya uwepo wa talakilishi chache ambazo hazikidhi
matumizi hayo lakini tayari wameagiza talakilishi hizo hivi karibuni wataanza
kutumia rasmi.
Hata hivyo amesema
matumizi ya digital katika shughuli za hospitali yanafaida kubwa ikiwemo
urahisi wa ukusanyaji wa mapato ambapo toka wameanza kutumia mfumo huo
wamebaini kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mapato katika hospitali ya makole.
Hivi karibuni
serikali kupitia wizara ya afya ilitoa tathmini ya utafiti uliofanywa na wizara
hiyo juu ya njia bora ya uhifadhi
takwimu ambapo walibaini kufanya vibaya kutokana na uhifadhi wa takwimu kwa njia ya makaratasi.
Na
Benard Filbert Dodoma FM
Comments
Post a Comment