
Ukosefu wa fedha
kutoka kwa wahisani na wadau mbalimbali imetajwa kuwa chanzo kikubwa
kinachopelekea kushindwa kukamilika kwa
miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilayani ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Hayo yamebainishwa
na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkhullo wakati akiwasilisha taarifa
ya miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018
kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa.
Amesema kuwa
katika robo ya tatu ya mwaka kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu
halmashauri ilitegemea kupokea kiasi cha shilingi Bilioni Moja Milioni Mia sita
ishirini na tano laki mbili na elfu
ishirini na tisa kutoka katika ruzuku ya maendeleo lakini hadi kufikia mwisho
wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri haijapokea pesa hizo.
Ameongeza kuwa
katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri
imepokea kiasi cha shilingi bilioni Moja Milioni Mia mbili sabini na nane laki
tatu elfu sitini na 2 mia sita sitini na nane.(1,278,362,668) pekee kwa ajili
ya miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa ambaye pia ni diwani wa kata ya
Kongwa White Zubery amewataka madiwani wote kuhakikisha wanasimamia fedha
zinazopatikana katika kata zao kupitia makusanyo mbalimbali ili kuendelea
kukuza uchumi wilayani humo.
NA ALFRED BULAHYA CHANZO :DODOMA FM
Comments
Post a Comment