Halmashauri ya
wilaya ya Bahi mkoani Dodoma imetakiwa kusimamia kikamilifu mpango wa matumizi
sahihi ya ardhi wilayani humo kwa kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu
yake katika kuleta maendeleo ya nchi.
Wito huo umetolewa
mapema wiki hii na BwanaPraygod Shao wakati akizungumza na taswira ya habari kwa
niaba ya Kamishina Mkuu Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ambapo
amesema kuwa licha ya serikali kutumia gharama nyingi kusimamia jambo hilo bado
kuna changamoto ya baadhi ya viongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo hali inayochangia kuendelea kuwepo kwa migogoro ya ardhi katika maeneo
mbalimbali.
Amesema kuwa
changamoto kubwa inayosababisha migogoro mingi ya ardhi ni suala la upimaji
kutotiliwa mkazo na kuwataka wahusika kama mabaraza ya ardhi kusimamia
kikamilifu suala hilo kwa kutumia kanuni na taratibu pamoja na kuwamilikisha
wahusika viwanja vyao baada ya kuvipima ili wanufaike na umiliki huo kama
kupewa mikopo na sekta za kifedha pindi wanapohitaji.
Aidha amewataka wananchi kuacha kukimbilia katika ngazi za juu kutafuta
suluhu wanapokumbana na migogoro na badala yake waanzie katika ngazi za chini
kwani ndiko mahali sahihi suala la ardhi linakoanza kusimamiwa huku akiyataka
mabaraza kusuluhisha migogoro na sio kutoa maamuzi ya kesi.
Na Alfred Bulahya DODOMA
FM
Comments
Post a Comment