Imeelezwa kuwa
sababu ya kutolewa kwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni kutokana na
kuonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wanaopata saratani huwa
inasababishwa na saratani ya mlango wa kizazi.
Hayo yameelezwa na
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma Dokta James Kihologwe wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo
amesema zaidi ya asilimia 50 ya wanawake
wanaougua saratani huwa chanzo chake ni saratani ya mlangio wa kizazi na
asilimia 70 husababishwa na virusi vya
HPV.
Dokta Kihologwe
amesema chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi si mpya na kwamba tayari
imekwishatolewa sehemu nyingi duniani na kwamba Tanzania imekwishatumika katika
Mkoa wa Kilimanjaro.
Wananchi wametakiwa
kufahamu kuwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni salama na kwamba binti
mwenye umri wa miaka 14 ndiye anayepaswa kupatiwa chanji hiyo kwa sasa.
Na
Mariam Matundu Dodoma
FM
Comments
Post a Comment