
Kampuni
zinazotengeneza vifaa vya ujenzi Dodoma zimeshauriwa kutumia fursa ya kufanya biashara katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia Dodoma.
Ushauri huo
umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati
akizungumzia juu ya maandalizi ya maonyesho kwa kampuni zinazotengeneza vifaa
vya ujenzi na samani za ndani pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi.
Akizungumza na
waandishi wa habari Kunambi amezitaka kampuni hizo kutumia fursa ya ujio wa
makao makuu kwa kujitambua, ili mashirika, taasisi na watu binafsi wanaojenga
Dodoma wafahamu ni bidhaa gani bora kwa ajili ya ujenzi.
Maonyesho hayo
yanafahamika kama Dodoma Builders Expo 2018, na amesisitiza kwamba fursa hiyo
ni kubwa na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waitumie kuonyesha bidhaa bora.
Kunambi amesema ni
kosa kulifananisha jiji la Dodoma na mikoa mingine nchini kwani linatakiwa
kufananishwa na Jiji la Nairobi Kenya na Pretoria Afrika ya Kusini.
Kwa upande wake
mratibu wa maonyesho hayo, Victor Simon amewataka
makandarasi wa jiji hili kuwatumia mafundi na vibarua wa Dodoma, na kuacha
tabia ya kutumia wale wa kutoka maeneo mengine.
Na Benard Filbert DODOMA FM
Comments
Post a Comment