Changamoto ya ukosefu wa wawekezaji wa miradi mikubwa ya
maendeleo katika viwanda, kilimo na miundo mbinu ni chanzo cha kushindwa kukua
kwa uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu hapa nchini.
Hayo yamebainishwa leo mjini Dodoma na Gavana wa benki kuu
ya Tanzania BOT Prof, Florence Luoga wakati akifungua warsha ya wadau wa sekta
ya fedha nchini iliyolenga kujadili mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo
ya uchumi.
Akisoma hotuba hiyo kwa niaba ya waziri wa fedha na
mipango Dkt Philpo Mpango prof Luoga amesema kuwa changamoto hizo ikiwa ni
pamoja na wananchi wengi kutofikiwa na huduma za fedha zimechangia mchango wa
fedha na bima kwenye pato la taifa ndani ya miaka 5 iliyopita kuendelea kubaki
asilimia 3.5 kiasi ambacho si cha kuridhisha.
Aidha katika kukabilia na changamoto hizo amewataka wadau
mbalimbali katika sekta ya fedha ikiwemo sekta ndogo ya benki na bima
kuhakikisha wanaboresha huduma kwa
wateja ili kuweza kupata faida itakayowawezesha kulipa kodi na kuongeza wigo wa
upatikanaji wa bima za kilimo hali ambayo itasaidia kuchangia maendeleo ya
taifa.
Awali akisoma hotuba ya katibu mkuu wizara ya fedha naibu
katibu mkuu Dkt Khatibu Kazungu amesema kuwa kwa mujibu wa utafiti wa shirika
la FINCECOP wa mwaka 2017 unaonyesha
kiwango cha matumizi ya fedha kinaongezeka kutokana na kuwepo kwa ubunifu
katika utoaji wa huduma ambapo tangu sekta ya fedha ilipoanzisha huduma ya
fedha kupitia simu za mikononi mwaka 2009 mpaka sasa imefikia asilimia 65
kutoka asilimia 15.9
Serikali inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya
fedha kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali na kuweka misingi imara ya
kuwezesha ukuaji , ushindani, na ufanisi katika sekta ya fedha.
Na Alfred Bulahya
Comments
Post a Comment