MKURUGENZI
wa halmashauri ya Chamwino Jijini Dodoma ATHUMAN MASASI amemvua madaraka ya ukatibu ndugu EKIA SHUMA
katika hospitali ya Wilaya hiyo kwa tuhuma za unyanyasaji dhidi ya
wafanyakazi.
Mkurugenzi
amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa
hospitali hiyo wakimtuhumu katibu huyo kuwanyanyasa watumishi,Kwa kutoa majibu
kwa namna anavyotaka na kutosikiliza shida za watumishi.
Akizungumza
katika kikao cha wafanyakazi baada ya kusikiliza malalamiko na kero za
watumishi mkurugenzi MASASI ametoa onyo pia kwa mlezi wa watumishi wa
kike(MATRONI)NEEMA MLULA kutokana na kulalamikiwa pia kuwanyanyasa watumishi.
Katika
hatua nyingine ameuagiza uongozi wa hospitali kujibu hoja 12 zilizotolewa na
mkaguzi wa hesabu za ndani wa halmashauri NGERANGERA TELESPHORD ambapo jumla ya
shilingi milioni 608.7 zimetumika bila ya kuwa na viambatanisho na hazikufuata
mfumo wa manunuzi ya umma.
Awali
mkaguzi TELESPHORD amewasilisha baadhi ya hoja zilizoanzia mwaka 2014 hadi
machi mwaka 2017.
Katika kikao hicho mkurugenzi huyo
amesikiliza kero na matatizo ya
watumishi hao ambapo wengi walilalamikia kutolipwa mishahara na
DCT,kutopandishwa vyeo kwa wakati jambo ambalo aliahidi kulifuatilia ili
kutatua changamoto hizo ikiwemo mtumishi mmoja aliyelalamikia kunyimwa ruhusa
ya kwenda masomoni ilihali alikuwa na ufadhili suala ambalo mkurugenzi alimtaka
katibu wa hospitali kulitolea ufafanuzi jambo hilo.
NA,MINDI JOSEPH DODOMA FM
Comments
Post a Comment