
Jumla ya shilingi milioni
60,152,487.65 zimelipwa na mahakama kama fidia kwa mashauri 16 yaliyo hakikiwa
na kuthibitishwa na mahakama baada ya kupokea fedha kutoka hazina kwa mwaka wa
fedha 2015/16 hadi 2016/17.
Waziri
wa katiba na sheria Prof Paramagamba Kabudi ameyasema hayo leo Bungeni Mjini
Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Rombo Mh. Joseph Selasini
alietaka kufahamu iwapo Serikali inazikumbuku za taarifa za watu waliotozwa
faini na kutakiwa kurejeshewa faini hizo.
Waziri
Kabudi amesema madai 24 yenye jumla ya shilingi milioni 87 yameshachambuliwa na
kufikishwa hazina tayari kwa kusubiri malipo wakati huohuo jumla ya madai 12
yenye thamani ya shilingi laki 9 yakiwa yamewasilishwa hazina tayari kwa
malipo.
Waziri
Kabudi amesema taarifa zote za wananchi wanaolipa faini zinatunzwa na mahakama
na hivyo urejeshwaji wa fedha hizo hutegemea upatikanaji wa nyaraka zinazo
thibitisha malipo ya faini kupokelewa na uwepo wa nakala ya hukumu.
Mh.
Kabudi amesema wapo baadhi ya wananchi wasiotambua haki yao ya kurejeshewa
faini ya fedha wanazotozwa baada ya kushinda kesi na hivyo ipo haja ya kutoa
elimu ili kutambua haki hiyo.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment