
Zaidi ya dola mil. 149.5
zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa kufua umeme kupitia mto
Malagarasi Ibamba two uliopo katika Mkoa wa Kigoma.
Waziri
wa Nishati Dr. Medard Kaleman ameyasema hayo leo bungeni mjini dodoma wakati
akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe aliehoji Serikali
imefikia wapi katika utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji katika mto Malagarasi
ambao ndio suluhisho kwa Mkoa wa Kigoma.
Dr.
Kalemani amesema mradi huo ulipangwa kutekelezwa mapema mwaka 2008 lakini
ukashindwa kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali na tayari mradi huo
umeingizwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 ambapo utekelezaji wake
unatarajiwa kuanza.
Akizungumzia
tatizo la kukatika kwa umeme Waziri Kalemani amesema tatizo hilo linatokana na
kasoro ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikijitokeza na tayari ufuatiliaji umekuwa
ukifanyika katika maeneo yanayobainika kuwa na tatizo la kukatika kwa umeme.
Katika
hatua nyingine naibu waziri wa nishati mh. Subira Mgalu amesema serikali
kupitia mradi wa urban eletification itaendelea kuyafikishia huduma ya nishati
ya umeme maeneo yaliyopo katika mamlaka za miji, manispaa pamoja na majiji.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment