WAZIRI MKUU AWASILISHA BAJETI YA MAKADIRIO YA OFISI YAKE NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019
Waziri mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Kasimu Majaliwa ameliomba Bunge kuridhia na
kuidhinisha fedha kiasi cha shilingi. Bil 124,958,230,698 kwa ajili ya
makadilio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya Bunge kwa
mwaka wa fedha 2018/19.
Waziri Mkuu amewasilisha leo makadirio ya mapato na
matumizi ya fedha ya ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge, kwa mwaka wa fedha
2018/2019 katika mkutano wa bunge la bajeti unaoendelea hapa mjini Dodoma.
Amesema kati
ya fedha hizo bil. 66,162,789,698 zitaelekezwa katika matumizi ya kawaida na bil.
58,791,841,000 zitaelekezwa katika matumizi ya maendeleo huku akiliomba Bunge
hilo kuidhinisha fedha kiasi cha sh. 125,521,100,000 kwa ajili ya mfuko wa Bunge.
Akielezea
mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr. John
Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka miwili iliyopita waziri mkuu Kasimu Majaliwa amesema serikali imefanikiwa
kujenga nchi yenye uchumi imara, kuimarisha ulinzi na usalama, kufufua shirika
la ndege la Tanznaia pamoja na kupambana
na dawa za kulevya.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria Mh. Mohamed Mchengelwa
amesema mpango wa bajeti ya ofisi ya waziri mkuu mwaka wa fedha 2018/19
umeainisha maeneo 23 ya vipaumbele ikiwemo kujenga uwezo wa serikali
kukabiliana na maafa.
NaPiusJayunga Dodoma FM
Comments
Post a Comment