Wavuvi wa samaki
waliopo kandokando ya bwawa la Mtera wameonywa kutowaachia watoto kutumia
mitubwi kutokana na madhara yanayopelekea
kuhatarisha maisha yao.
Wito huo umetolewa na Diwani wa kata ya mtera BW,AMONI KODI
mapema leo kufuatia tukio la hivi karibuni ambalo limesababisha kifo cha mtoto
mmoja aliyepoteza maisha,baada ya mtubwi aliokuwa akichezea kupinduka ndani ya
bwawa hilo.
Akizungumza kuelekea
ziara na wakazi wa vijiji vya Chibwegere na mtera wanaojishughulisha na uvuvi wa samaki,amesema
lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa
wavuvi hao kuweka walinzi ili kudhibiti watoto kuchezea vyombo hivyo vya uvuvi.
BW,KODI ameongeza kuwa
wazazi wanatakiwa kuwalinda watoto wao pamoja na kutowaruhusu kuchezea mitumbwi
hiyo na amewasihi wakazi hao waliopo kandokando ya bwawa kuhakikisha wanaweka
walinzi makini watakaosaidia ulinzi wa
watoto.
Hata hivyo amesema kuwa mbali na madhara ya kuachwa kwa mitubwi
hiyo,pia hatari nyingine inayoweza kutokea ni pamoja na kushambuliwa
na viboko ambao wamekuwa wengi ndani ya bwawa hilo la Mtera.
Na,Mindi Joseph
Chanzo Dodoma FM
Comments
Post a Comment