Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika imeagiza
kurudishwa kazini watumishi wote wa Umma waliofukuzwa kimakosa ikiwemo wale
walioishia darasa la saba.
Waziri
Mkuchika ametoa maelekezo hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akitoa tamko la
Serikali juu ya watumishi walio ajiriwa Serikalini kabla ya tarehe 20 mwezi mei
mwaka 2004 kurudishwa kazini baada ya kuondolewa kutokana na kasoro mbalimbali
zilizojitokeza.
Waziri
Mkuchika amesema watumishi hao watalipwa mishahara yao katika kipindi chote
walipoondolewa kazini na kuendelea na ajira zao hadi watakapostaafu kwa mujibu
wa sheria
Amesema
uamzi huo hautahusisha makundi ya watumishi waliowasilisha vyeti vya kugushi
hata kabla ya 2004, watumishi waliokuwepo katika ajira kabla ya tarehe 20
mei mwaka 2004 ambao taarifa zao
zilikuwa za uongo pamoja na watendaji wakuu wa idara waliohusika kuajiri watu
wasiokuwa na sifa watachukuliwa hatua za kisheria.
Kwa
mujibu wa waziri mkuchika, utekelezaji wa ajira katika utumishi wa umma tangu
kuanza kutumika kwa miundo mipya, umekuwa na tafisri tofauti na kufuatia hali
hiyo Serikali ilitoa maelekezo kwa waajiri kusimamisha mishahara kwa watumishi
walio ajiriwa baada ya tarehe. 20 mwezi mei 2004 wakiwa hawana sifa ya kufaulu
katika mitihani yao ya kidato cha nne.
Na Pius Jayunga Dodoma Fm
Comments
Post a Comment