
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Dodoma, Gilles Muroto amewataka wananchi wa Dodoma waliopotelewa na pikipiki
wafike kituo cha polisi kwa ajili ya kuzitambua pikipiki zilizoshikiliwa.
Kamanda Muroto amemweleza
Mkuu wa Mkoa, Dk Binilith Mahenge kuwa jeshi hilo limefanya doria na misako ya
wahalifu maeneo ya manispaa ya Dodoma na mji mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwa.
Amesema, katika
doria wamemkamata mfanyabiashara mkazi wa Nkuhungu Manispaa ya Dodoma, Josephat
Komba mwenye umri wa miaka 28 akiwa na pikipiki tano aina ya boxer ambazo ni za
wizi.
Pia kamanda Muroto
amesema wamemkamata Mkazi wa Chang'ombe, manispaa ya Dodoma, Nassoro Masangu
mwenye umri wa miaka 27 aliyetafutwa muda mrefu akidaiwa kuvunja nyumba za watu
usiku na kubaka wanawake.
Jeshi hilo pia limekamata
watuhumiwa wengine watano wakiwa na pikipiki tatu kwa unyang'anyi kwa kutumia
pikipiki kupora na kutoroka baada ya kufanya matukio hayo.
Watuhumiwa hao ni
Idd Yusufu (22) mkazi wa Chinangali, Ramadhani Juma (21) wa Hazina, Maneno Jonas
(20) wa Chang'ombe, Mohamed Mbinga (22) wa Chinangali na Nzoyi Peter (24) wa
Nkuhungu.
Na Zania
Miraji
Dodoma FM
Comments
Post a Comment