WATU MILIONI 600 HUUGUA NA ZAIDI YA WATU LAKI 4 HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KUTOKANA NA CHAKULA KISISCHOKUWA SALAMA
Takribani
watu milioni mia sita duniani kila mwaka huugua magonjwa mbalimbali huku wengine laki nne na elfu ishirini hupoteza
maisha kutokana na kula chakula kisichokuwa salama.
Hayo
yamebainishwa leo na kaimu mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Nassoro Mzee
wakati akizungumza kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa kwenye ufunguzi wa
mafunzo maalumu kwa wataalamu wa afya kutoka katika halmashauri 9 za mkoa wa
Dodoma yenge lengo la kuwawezesha wataalamu kuongeza uelewa katika kuandaa
taarifa za magonjwa yatokanayo na chakula.
Dkt
Mzee amesema kuwa madhara yatokanayo na chakula kama kuhara damu,homa ya
matumbo na kipindupindu ,yamekuwa ni tatizo kubwa dunia kwani yamekuwa yakisababisha kuzorotesha
uchumi wa nchi na hupelekea vifo na athari kubwa kwa jamii kutokana na baadhi
ya wagonjwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Aidha
ametaja sababu mbalimbali zinazochangia uwepo wa chakula kisicho kuwa salama
kuwa ni pamoja na jamii kutozingatia kanuni za ubora za uzalishaji kuanzia
ngazi za mashambani, usafirishaji ,usindikaji na utayarishaji wa chakula hivyo
ni vyema jamii ikawa na uangalizi madhubuti ili kuepusha madhara yatokanayo na
chakula.
Kwa
upande wake Meneja mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya kati dkt
Engelbert Bilashomoka amesema kuwa mkoa
wa Dodoma umeonekana kuwa na magonjwa mengi yatokanayo na chakula licha ya
kuwepo kwa changamoto ya kutotumwa taarifa kwa mamlaka hiyo hivyo amewataka
wataalamu kuhakikisha wanatoa taarifa ili kuendelea kupambana na tatizo hilo.
Mpango
wa kukusanya magonjwa yatokanayo na chakula ulianzishwa hapa nchini mwaka 2008
kwa lengo kufanya ufatiliaji mapema ili kuhakikisha magonjwa haya yanatokomezwa
na amewataka waandaaji wa vyakula katika maeneo mbalimbali kuzingatia kanuni na
taratibu sahihi za uaandaaji wa vyakula kama kunawa mikono na sabuni baada ya
kutoka chooni ,kabla ya kuaanda na kabla
ya kula chakula.
Na Alfred Bulahya Dodoma FM
Comments
Post a Comment