Watanzania wametakiwa kujenga mshikamano katika
kukemea mambo yanayokinzana na maadili ya kitanzania ili kuendelea kudumisha
mila na desturi za nchi.
Wito huo umetolewa leo na afisa
utamaduni wa manispaa ya Dodoma bw Desdeli Kuzenza wakati akizungumza na Dodoma
FM kupitia kipindi cha Taswira ya Habari .
Bwana Desdeli ameyasema hayo ikiwa
ni siku chache tu tangu Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kukemea kitendo cha wanajamii kukiuka maadili ya uvaaji.
Amesema kuwa
umefika wakati sasa wa Kuacha kuiga mambo yasiyo na tija kutoka katika mataifa
mengine na badala yake kuwepo na desturi ya kuhakikisha jamii inakuwa na
ushirikiano katika kukemea suala la uvaaji wa nguzo zisizokuwa na maadili ya
kitanzania.
Aidha ameitaka
jamii kutumia vizuri utandawazi na mitandao ya kijamii ili kujiletea manufaa
kwani baadhi ya vijana wamekua wakiiga mambo mbalimbali kutoka mitandaoni jambo
ambalo linasababisha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.
Hivi karibuni Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt John Pombe Magufuli alikemea vikali suala la uvaaji nguo
zisizoendana na maadali ya kitanzania kwani kufanya hvyo ni kinyume na mila na
desturi za Watanzania.
Na Alfred Bulahya Dodoma
FM
Comments
Post a Comment