Wanawake Mkoani
Dodoma wamehimizwa kuendelea kuunda vikundi vitakavyowasaidia kupata asilimia
tano zinazotolewa na halimashauri ya manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuondokana
na dhana ya kuwa tegemezi kwa kuleta
maendeleo.
Wito huo umetolewa
na Diwani wa viti maalum manispaa ya Dodoma FATUMA RAMADHANI ZOLO wakati akizungumza na kituo
hiki ambapo amesema kwa kushirikiana na madiwani wa viti maalum wamekuwa na
jukumu la kufika katika kata 41 kwa
kupelekea miradi mbalimbali kwa wanawake
ikiwa ni pamoja na ufugaji wa kuku.
BI,FATUMA RAMADHANI
ZOLO ameongeza kuwa wameweka mikakati ya
kuwasaidia wanawake kwa kuwawezesha kupata asilimia tano zinazotolewa na
manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuanzisha biashara zitakazowasaidia kujipatia
kipato.
Katika hatua
nyingine amebainisha kuwa tayari wamefanikiwa kupeleka miradi ya ufugaji wa
kuku wa kienyeji,ufugaji wa mbuzi pamoja na kuwapatia pesa kwa lengo la
kuendeleza vikundi vyao na amewahimiza
kuendelea kuunda vikundi vya ujasiriamali hususani vijijni.
Aidha kutokana na
serikali kuweka asilimia ya hamsini kwa hamsini kwa wanawake na wanaume
imepelekea kupunguza wanawake wengi kuwa tegemezi kutokana na elimu inayotolewa
ya kuunda vikundi endelevu na vinavyowapatia manufaa.
Na,Mindi
Joseph Chanzo Dodoma FM
Comments
Post a Comment