Wakunga wa jadi
nchini wamehimizwa kutowachelewesha akina mama wajawazito katika vituo vya afya ili wajifungue salama.
Akizungumza na Dodoma
FM mapema leo Msaidizi wa Mratibu wa afya ya Mama na mtoto Mkoa wa Dodoma Bi Liberia
Gambosi amesema Baadhi ya wakunga wa jadi hutoa huduma za kuzalisha akina mama
majumbani na kupelekea wengi wao hutokwa na damu nyingi na kupoteza maisha.
Bi.Gambosi amesema
akina mama wasiwategemee wakunga wa jadi bali wafike katika zahanati na vituo
vya afya kwa ajili ya uangalizi wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Bi
Dina Msesa ambae ni Afisa muuguzi amesema Upungufu wa manesi na wauguzi katika
vituo vya afya ni chanzo kinacho tajwa akina mama kuwatafuta wakunga wa jadi.
Na,
Sadoki Mabawa Chanzo;
Dodoma FM.
Comments
Post a Comment