Wananchi
wameshauriwa kutoa taarifa mapema kwa
watu wao wa karibu pindi wanapogundua wana
maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI.
Ushauri huo umetolewa na katibu wa baraza la taifa la watu wanaoishi
na maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoa wa Dodoma Bwana Enock Mshumbusi wakati
akizungumza na Dodoma FM na kusema kuwa utoaji wa taarifa mapema ni vizuri
kwani unasaidia mtu kupata huduma kwa urahisi.
Sambamba na hayo bwana Mshumbusi amesema kuwa kitendo cha
kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI ni kusaidia kuongeza kinga
ya mwili.
Hata hivyo, Bwana Mshumbusi amesema kuwa kwa mtu ambaye ameanza
kutumia dawa anatakiwa kuwa na msimamizi ambaye atamsaidia huku akisema
kuwa baadhi ya wanajamii wamekuwa wagumu
kuwasaidia watu walio athirika kwani bado wanaamini ukishirikiana.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya takwimu nchini mwaka 2017
alinukuliwa akisema mkoa wa njombe una asilimia 11.5 ya watu wanaoishi na
ugonjwa huo huku Zanzibar ikiwa chini ya asilimia 1.
Na
Benard Filbert
Dodoma FM
Comments
Post a Comment