Wananchi wa kata ya
Msamalo iliyoko halmashauri ya wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wametakiwa
kuacha tabia ya kuitegemea serikali kutenda kila jambo na badala yake
wahakikishe wanajitokeza kujitolea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo
ili kuendelea kujiletea vipato.
Wito huo umetolewa
leo na diwani wa kata ya Msamalo bw Elias Wilson Kawia wakati akizungumza na
Dodoma FM ambapo amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kutambua
mahitaji yake hivyo ni vyema kila mmoja akainuka kufanya kazi pindi
anapohitajika na kuacha kuitegemea serikali ifanye kila jambo.
Ameongeza kuwa
wakati wizara mbalimbali zikiendelea kuhamia mkoani Dodoma jamii inapaswa
kutumia fursa hiyo kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zitakazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi
kama kujikita katika kilimo cha Alzeti na Mtama jambo ambalo litawasaidia
kupata mapato kupitia mazao hayo.
Aidha amepongeza
wananchi wa kata hiyo kwa ushirikiano wanaoutoa kwa viongozi wao na amewaomba
kuendelea kuunga mkono juhudi mbalmbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya
tano huku akiwataka kuhakikisha wanatunza kwa umakini mazao ya vyakula ili
kutokomeza adui njaa hapa nchini.
Na Alfred
Bulahya Chanzo:
Dodoma FM
Comments
Post a Comment