Wakazi
wa Jiji la Dodoma wameaswa kuacha kuilalamikia serikali kuwa imeshindwa kutoa
ajira kwa vijana badala yake wajikite
kuwekeza katika masomo ya ufundi ya muda mfupi ili kupunguza tatizo
hilo.
Wito
huo umetolewa na mkuu wa chuo cha VETA Dodoma Ramadhani Mataka wakati akizungumza na Dodoma FM
kupitia kipindi cha Taswira ya habari juu ya namna ya kuondoa tatizo la ajira
kwa vijana.
Bwana
Mataka amesema kuwa baadhi ya watanzania wamekuwa wakilalamikia serikali kuwa
haitoi ajira badala ya kujiongeza kusoma hata kozi fupi zitakazowawezesha
kujipatia vipato.
Amesema
kuwa wakati Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DKT John Pombe Magufuli akisisitiza
uwepo wa serikali ya viwanda ni lazima watu wahakikishe wanasoma mafunzo ya
ufundi wa fani mbalimbali ili kuviwezesha viwanda kufanya kazi kwa ufanisi na
sio kutegemea watu wa mataifa mengine waje kufanya kazi katika viwanda hivyo.
Ameongeza
kuwa lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa vyuo vya VETA ni kutokana na kuwepo
kwa changamoto ya upungufu wa ajira nchini na moja ya majukumu yake ni
kuhakikisha vinatoa mafunzo ya ufundi ili kuwawezesha vijana wanaotoka vyuoni
wawe na maarifa yatakayowasaidia kupata ajira katika maeneo mbalimbali au
kujiajiri wenyewe.
Katika
hatua nyingine bw Mataka amesema wakati serikali ikiendelea kuhamia Dodoma
waalimu waliopata nafasi ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa chuo cha VETA Dodoma
wanatakiwa kuhakikisha wanatoa mafunzo yenye uwezo wa kuwasaidia wawapo mitaani
kwani wengi wao ni watoto wanaotoka katika familia duni.
Na
Alfred Bulahya Dodoma FM
Comments
Post a Comment