DIWANI wa kata ya Mtera wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma
amewataka wananchi wa vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo kuacha kuuza mazao yao
yakiwa bado shambani kwa walanguzi badala yake Wahifadhi chakula cha kutosha
ili kuepukana na baa la Njaa.
Akizungumza na Dodoma FM mapema hii leo Diwani wa kata
hiyo Bwana AMON KODI amewaasa wananchi kutokufanya makosa kama walivyofanya mwaka 2016 na 2017 ambapo
baadhi ya wakulima walidiriki kubadilishana debe moja la mtama na mahindi kwa
bia moja baada ya kuvuna mavuno mengi.
Bwana KODI ameongeza kuwa mazao ambayo wananchi wamevuna mwaka huu ni
muhimu kuyahifadhi ili kuwasaidia katika kipindi chote cha kiangazi.
Aidha amebainisha kuwa
baada ya kipindi cha mvua kuisha msimu wake wananchi wanatarajia kuanza
ujenzi wa vyoo kutokana na vile vilivyokuwepo awali kuanguka na mvua zilizokuwa zikinyesha.
Na,Mindi Joseph Chanzo
Dodoma FM
Comments
Post a Comment