Wakazi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuachana na ngono zembe ili kuepukana na magonjwa yasababishwayo na ngono zisizo salama.
Akizungumza na Dodoma
FM daktari MUZNA UJUDI kutoka hospitali ya rufaa mkoani hapa amesema kwasasa magonjwa ya ngono yamekuwa
yakiwakabili watu wengi hususani ugonjwa wa homa ya INI ambao umekuwa ukiwapata watu wengi kupitia ngonozembe.
Dokta MUZNA amesema
mbali na kuwa ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya ngonozembe pia mtu anaweza
kuupata kwa kuongezewa damu ya mtu ambae tayari ana virusi vya ugonjwa huo (HEPATATICS B) pamoja na kuchangia vitu vya
ncha kali kama vile sindano kwaajili ya matibabu.
Pia ameeleza dalili
za mwanzo za ugonjwa wa homa ya ini kuwa ni kubadilika kwa rangi ya macho
kutoka katika hali ya kawaida na kuwa na unjano,kupata maumivu ya tumbo,
kukojoa mkojo wenye rangi ya njano iliyokolea pamoja na mwili kuwa mchovu.
Aidha imeonekana
kuwa dalili za ugonjwa huu zinaweza kutoonekana kabisa kwa kipindi cha mwanzo
unapoambukizwa na kuja kuibuka wakati ukiwa tayari umeharibu INI jambo ambalo limepelekea
mganga huyo kuwataka wakazi wa DODOMA kujihadhali kwa kupima afya zao mapema.
Sanjari na hayo ameitaka
jamii kuachana na ngonozembe badala yake watumie kinga pamoja na kuwa waaminifu
kwa kuwa na mpenzi mmoja ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ambayo
yanaweza kuepukika.
Na
Anipha Ramadhan Dodoma FM
Comments
Post a Comment