
Wananchi wa mtaa wa Kisabuje uliopo Area A Manispaaa
ya Dodoma wameiomba halmashauri ya manispaa ya Dodoma kuwahamishia Dampo lililopo katikati ya makazi yao ambalo
limekuwa likiwakera kwa kipindi cha takribani
miaka miwili.
Wakizungumza na Dodoma FM wakazi hao wamedai kuwa Dampo hilo limekuwa changamoto kwao
kutokana na harufu inayotokana na taka zinazotupwa hapo kukaa muda mrefu bila
kupelekwa katika eneo husika.
Aidha wamedai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa
ya mlipuko kwani wadudu wasambazao magonjwa hayo wanaweza kusafirisha uchafu
kutoka katika taka hizo na kupeleka
katika vyombo wanavyotumia kwa matumizi yao.
Akijibu tuhma hizo Mwenyekiti wa mtaa huo Bw.UHURU CHIWARIGO
amesema tayari taarifa hiyo
ameipeleka manispaa na kwa afisa afya ambapo hadi sasa anasubiri
mwitikio kutoka kwa ili kuhamishia taka hizo katika eneo lililopo Dampo la Sokoine.
Bw. Chiwarigo amesema moja kati ya changamoto ambayo inawatatiza
katika mtaa huo ni kutofika kwa wakati kwa
magari yanayobeba taka jambo ambalo linapelekea kuhifadhi taka kwa muda
mrefu katika eneo hilo ambalo ni hatarishi kwa maisha ya wananchi.
Hata hivyo amewataka wananchi wake kuwa wavumilivu kwa
kipindi hiki kifupi na kusema kuwa tayari zoezi hilo lipo kwenye mikakati ambapo
wanasubiria halmashauri kuleta kijiko kwa ajili ya kuziondoa taka hizo.
Na ANIPHA RAMADHAN CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment