Wananchi
wa mtaa wa chiloloma kata ya Hombolo manispaa ya Dodoma wametakiwa kuacha kufumbia macho
vitendo vya kiuhalifu kama wizi unyanyasaji na ukatili katika jamii badala yake watoe ushirikiano kwa vyombo
husika kwa kutoa taarifa.
Wito huo umetolewa leo
na mwenyekiti wa mtaa wa Chiloloma Gerald Mtagwa wakati akizungumza na Taswira ya habari
ambapo amesema kuwa mwananchi anapoona vitendo vya uhalifu anatakiwa kutoa
taarifa kwa vyombo husika ili vitendo hivyo viweze kushugulikiwa.
Amesema kuwa
tunapozungumzia Tanzania ni nchi yenye amani ni usalama kwanza hivyo ni vyema jamii ikajilinda kwa kutoa
taarifa mapema hata kama uhalifu unafanywa na ndugu yako kwani kufumbia macho
suala hilo ni kuendeleza uhalifu.
Aidha katika
kuendelea kupambana na suala la uhalifu nchini Mtagwa amezitaja changamoto
wanazokabiliana nazo wakiwa katika suala la ulinzi kuwa ni pamoja na ukosefu wa
vifaa mbalimbali vya ulinzi ambapo ameliomba jeshi la polisi kutafuta namna ya
kutoa mafunzo sahihi ya utumiaji wa silaha kwa polisi jamii hasa katika maeneo
ambayo matukio ya uhalifu yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.
Na Alfred Bulahya Dodoma
FM
Comments
Post a Comment