Wananchi
mkoani Dodoma wametakiwa kuacha tabia ya kuuziana maeneo bila kufuata
utaratibu kutoka kwa viongozi
wanaohusika na kitengo hicho.
Wito huo umetolewa
na Afisa Habari wa Halmashauri ya manispaa ya Dodoma Bw.RAMADHANI JUMA wakati
akizungumza na Dodoma FM ambapo amesema tangu sarikali ilipohamishia shughuli
zake mkoani hapa kumekuwa na migogoro ya
ardhi.
Bw. Ramadhani
amesema halmashauri ya manispaa ya Dodoma ilikabidhiwa shuguli za aridhi
rasmi tangu ilipovunjwa mamlaka ya
ustawishaji Makao makuu CDA mwezi MEI mwaka
jana ambapo hadi sasa wamefanikiwa kwa
wasatani kutatua migogoro ya ardhi kwa baadhi ya maeneo katika manispaa ya
Dodoma.
Kwa kipindi hiki
ambacho manispaa imekabidhiwa shughuli za aridhii TAKWIMU zinaonesha kuwepo kwa
migogoro ya aridhi 982 Tangu may mwaka jana hadi february mwaka huu
ambapo hadi sasa wametatua takribani migogoro 411 huku mingine 572
ikishughulikiwa katika ngazi tofauti.
Aidha ameongeza
kuwa wananchi wamechukulia fursa ya serikali kuhamia mkoani hapa kama kigezo
cha wao kujipatia kipato kupitia maeneo waliyo nayo kwa kuuziana wao pamoja na
wageni wanaohamia bila kufuata kanuni.
Afisa habari huyo
amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Dodoma kuwa wameweka mikakati ya mipamgo miji ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa
kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi.
Na
ANIPHA RAMADHAN CHANZO:DODOMA FM
Comments
Post a Comment