Katika hatua ya
kuboresha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule ya msingi Chamwino shule
hiyo imeanzisha utaratibu wa kupata
chakula cha mchana kwa wanafunzi wa darasa la saba ili kuwajengea uwezo wa
kuendelea na masomo ya ziada shuleni hapo.
Akizungumza na
Dodoma fm ofisini kwake mjumbe wa kamati ya shule ya msingi Chamwino ambaye pia
ni kaimu mwenyekiti wa mtaa wa nduka jijini Dodoma bwana KASIMU YUSUFU amesema
shule hiyo ilifikia makubaliano hayo kupitia vikao mbalimbali walivyokaa baina
ya wazazi kamati ya shule na serikali ya mtaa.
Amesema kwa kuanza
wameanza na darasa la saba kwa kuzingatia wao ndio wanaokabiliwa na mitihani
migumu ikiwemo mitihani ya kitaifa.
Wakati huo huo Bwana YUSUFU amempongeza mbunge wa jimbo la
Dodoma mjini mheshimiwa ANTONI MAVUMDE kwa kuipatia shule hiyo ya chamwino
komputa ikiwa ni kwa ajili ya kutunzia kumbukumbu ili kuendana na mfumo wa
kisasa japo amesema bado shule hiyo
inahuitaji wa printa.
Aidha amewaomba
wananchi wa Chamwino na wadau wa elimu kuendelea kutoa ushirikiano pale
wanapowahitaji.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE DODOMA FM
Comments
Post a Comment