Halmashauri zote Nchini zimeagizwa
kuwahamishia walimu walio na uwezo wa kufundisha wanafunzi walio na ulemavu
wakiwemo walio na usonji katika shule zilizo na uhitaji hadi ifikapo mwezi
Desemba mwaka huu.
Naibu
Waziri wa TAMISEM Mh. Joseph Kakunda ametoa maagizo hayo leo Bungeni Mjini
Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa kuteuliwa Mh. Salma Rashid Kikwete aliehoji
Serikali inawasaidiaje watoto wenye usonji wapate elimu, pamoja na idadi ya
walimu wao iwapo wanatosheleza.
Mh.
Kakunda amesema mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi 1416 walio na tatizo la
usonji huku idadi ya walimu wao wakiwa 157 walioko katika shule 18 za msingi Nchini
idadi ambayo ni ndogo kulingana na idadi ya wanafunzi walio na uhitaji maalumu.
Amesema
mkakati wa Serikali ni kuwatambua watoto walio na tatizo la usonji Nchini kote
ili kuwapatia haki ya elimu kama ilivyo kwa watoto wengine huku mtoto mmoja
alie na usonji akihitaji kufundishwa na mwalimu mmoja lakini kutokana na upungufu
wa walimu inalazimu mwalimu mmoja kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi.
Kutokana
na upungufu wa walimu walio bobea katika ufundishaji kwa wanafunzi walio na
ulemavu Mbunge Suzan Lyimo ameshauri kutoa kipaumbele cha ajira kwa walimu
walio hitimu mafunzo hayo wakiwemo waliosomea katika chuo cha viziwi kilichopo Mkoani
Tabora huku Naibu Waziri Kkunda akiahidi kutoa kipaumbelea cha ajira kwa walimu
hao.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma FM
Comments
Post a Comment