
Uhaba wa vyumba vya madarasa ni miongoni mwa changamoto inayoikabili shule ya msingi Mapinduzi iliyopo Kijiji cha Nzali kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma hali inayopelekea wanafunzi kusomea chini ya mbuyu.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa shule hiyo Bi Subira Salimu Wakati wadau wa shirika la ACTION AID walipotembela shuleni hapo wakiwa katika
shughuli mbalimbali za kuelekea kilele cha maadhimisho ya juma la
Elimu Duniani.
Amesema
shule yake ina jumla ya wanafunzi 202 kuanzia darasa la kwanza hadi
la saba sawa na wasichana 108 na wavulana 94 huku ikiwa na
vyumba 4 vya madarasa hali inayopeleka
darasa la pili kusomea chini ya mbuyu.
Aidha amesema
uhaba wa matundu ya vyoo pia ni changamoto inayowakabili wanafunzi hao, ambapo
amedai shule ina matundu ya vyoo sita kwa wanaume na wanawake hali
inayopelea kusubiriana wakati wa kujisaidia.
Akizungumza
katika hadhara hiyo Kaimu Afisa Elimu Wilayani hapo Bi Amina Mussa
amewataka wazazi kuacha kuwashinikiza watoto wao kutofanya vizuri katika
mitihani yao ya kuhitimu na kudai kuwa watoto wa kike wanahitaji kupata Elimu
sawa na watoto wa kiume.
Naye
Katibu wa Jukwaa la Wanawake na Wakulima wilayani hapo JUWACHA lilipo chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la
ACTION AID Sophia Bhoke amesema
wao kama JUWACHA wamefanya
tathimini ya pima kadi na matokeo katika sekta ya Elimu wamegundua uhaba wa
walimu ni tatizo kubwa kwa baadhi ya shule.
Hata
hivyo wazazi wa wanafunzi akiwemo Magrent Mtango amesema
changamoto inayowakumba watoto wao ni pamoja na uhaba wa vitabu huku wanafunzi wakitaja changamoto wananzo kutana
nazo pindi wawapo shuleni.
Madhamisho
ya kilele cha Juma la Elimu Duniani hufanyika aprili 27 kila
mwaka.
Na
Alfred Bulahya DODOMA FM
Comments
Post a Comment