Wakulima mkoani Dodoma wameshauriwa
kuvuna mazao ya nafaka yakiwa katika hali ya kukomaa ili kuyaepusha kushambuliwa na wadudu
wajulikanao kama dumusi pindi watakapo
yahifadhi kwa ajili ya chakula.
Ushauri huo umetolewa na Afisa kilimo
mkoani Dodoma Bw. Benard Abraham wakati akizungumza na Taswira ya Habari ambapo
amesema kuwa kwa kipindi hiki ambacho wakulima wanaelekea kuvuna ni vema wakatumia
njia salama za uhifadhi wa mazao ili kuhakikisha yanakaa kwa muda mrefu bila
kubunguliwa na wadudu.
Bw. Abraham amesema miongoni mwa sababu
inayofanya mazao ya nafaka kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika ni kuhakikisha
yanakauka vizuri na kuondokana na hali ya unyevunyevu na kuhifadhi katika mifuko ,maghala pamoja na vihenge.
Aidha amewataka wananchi kutotumia dawa
kama njia ya kuzuia wadudu wanao haribu mazao kutokana na dawa hizo kuwa na
madhara ikiwa zitatumika kinyume na taratibu
badala yake watumie njia salama ambayo ni mifuko, maghala pamoja na vihenge.
Pamoja na hayo Afisa Kilimo huyo amewataka
wakulima kufuatilia mashamba yao na kutopuuzia pale wanapoona kuna dosari
katika mimea ikiwa ni kuondokana na dhana ya kuwalalamikia maafisa ugani kuwa
hawawatembelei katika mashamba yao na badala yake watoe ushirikiano kwa maafisa
ugani wao.
Na ANIPHA RAMADHAN DODOMA FM
Comments
Post a Comment