Kuelekea
maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi mei mosi 2018 imebainika kuwa idadi kubwa ya waajiri
hawatekelezi ipasavyo sheria ya kazi namba 8,ya mwaka 2006 kwa kutoa mikataba
kwa waajiriwa.
Hayo yamelezwa na
kaimu katibu wa chama cha wafanyakazi TUCTA makao makuu bwana Ramadhani Mwendwa
wakati akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu.
Bwana Mwendwa
amesema waajiri wengi hususani katika taasisi binafsi hawafuati sheria hiyo
ambayo inamtaka muajiri kuhakikisha anatoa mkataba kwa muajiriwa wake huku
akiamini sikukuu hiyo inasaidia kuhamasisha waajiri kuzingatia kanuni na sheria
za kazi na mahusiano.
Hata hivyo amesema
kila mwaka chama cha wafanyakazi katika maadhimisho hayo wamekuwa wakijitahidi
kufikisha malalamiko ya wafanyakazi ikiwepo suala la nyongeza ya mshahara kwa
wafanyakazi na kupandishwa madaraja kazini.
Bwana Mwendwa
amewataka wafanyakazi kujitokeza katika sherehe hizo kwani ni njia pekee ya
kukutana na viongozi wa serikali na kuwasilisha matatizo yao.
Maadhimisho ya
meimosi yatafanyika katika mkoa wa iringa siku ya kesho ambapo Rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo.
Na
Benard Filbert
Dodoma FM
Comments
Post a Comment