
Wakazi wa Manispaa
ya Dodoma wameshauriwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya wanaopewa ili kujikinga
na ugonjwa wa malaria.
Rai hiyo imetolewa
leo na Daktari wa zahanati iliyopo chini ya chama cha uzazi na malezi bora
Tanzania (UMATI) iliyopo kata ya chamwino manispaa ya Dodoma Daktari JORAM
ELIKANA wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya namna bora ya kudhibiti ugonjwa
wa malaria.
Daktari Joram amesema
kuwa kama jamii itazingatia ushauri na maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya
kwa kutumia vyandarua wakati wa kulala na usafi wa mazingira ni dhahili kuwa ugonjwa wa maralia utapungua kama sio kuisha
kabisa kama ilivyo dhamira ya serikali.
Daktari ELIKANA amesema pamoja na kuwepo kwa baadhi ya
wahudumu wa afya kuwauzia dawa za maralia wagonjwa na wengine kutumia lugha mbaya pindi wanapowahudumia wagonjwa
jambo jingine amesema ni ucheleweshaji wa usambazaji wa dawa na vifaa tiba
katika vituo vya Afya jambo ambalo linaashiria kupunguza kasi ya mapambano
dhidi ya ugonjwa wa maralia.
Hivi karibuni
waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto UMMY
MWALIMU amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kote nchini kuandika ubao wa
matangazo katika hospitali utakaomjulisha mwananchi kuwa huduma ya malaria
inatolewa bure na kuwa ni kipimo kipi kinatumika kupima malaria huku waganga
wakuu wa wilaya na zahanati wakiagizwa kutoa namba zao za simu kwa ajili ya
kupokea malalamiko ya wagonjwa iwapo watahudumiwa tofauti na maelekezo kutoka
kwa wahudumu.
Na
RWEIKIZA KATEBALIRWE Chanzo:DODOMA FM
Comments
Post a Comment