Waajiri wa wafanyakazi wa ndani wametakiwa
kuacha tabia ya kuwapiga,kuwanyanyasa pamoja na kuwatumikisha kazi zisizostahili kutokana
na sheria ya ajira kuzuia kuwepo kwa vitendo hivyo Kwani wafanyakazi hao wana haki kama waajiriwa
wengine.
Rai hiyo imetolewa na Bwana CHRISPO
RWILA ambaye ni mwanasheria kutoka Taasisi isiyokuwa ya kiserikali wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya
haki na wajibu wa Wafanyakazi wa ndani.
Bwana Chrispo amesema Kwa mujibu wa
sheria ya ajira ya mwaka 2004 wafanyakazi wa ndani wana haki ya kuthaminiwa na
kupewa mikataba.
Aidha Bwana RWILA ameongeza kuwa endapo
mfanyakazi wa ndani akifanyiwa ukatili au ukiukwaji wa mkataba dhidi ya muajiri wake ana
haki ya kwenda kumshitaki mahakamani ili kuweza kupata haki yake.
Taswira ya habari imefanikiwa
kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa
ndani na akabainisha changamoto kubwa
anayokumbana nayo ni kupigwa na muajiri wake huku akipewa kazi ambazo hazistahili.
Na,Mindi
Joseph Chanzo
Dodoma FM
Comments
Post a Comment