Watanzania wameshauriwa
kupunguza kula vyakula vya aina ya Fat ili kupunguza uwezekano wa kupata taizo
la tezi dume linalowapata wanaume.
Rai
hiyo imetolewa na Daktari Bingwa wa upasuaji upande wa mfumo wa mkojo pamoja na magonjwa ya akina baba Dk. Remmy kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa mjini Dodoma wakati
akizungumza na Dodoma FM kupitia kipindi cha Dodoma Live.
Dokta
Remmy amesema upunguzaji wa ulaji wa vyakula aina ya Fat pamoja na kufanya
mazoezi kutasaidia kupunguza uwezekano wa kupata tezi dume.
Dk.
Remmy amesema ni vizuri mtu anapokutwa na tatizo akawahi katika kituo cha afya
kupata matibabu kwani watu wengi wanapoteza
maisha kutokana na tatizo la TEZI DUME na hiii ni kutokana na baadhi yao
kutokuwa na elimu juu ya tatizo hilo.
Amebainisha
kuwa baadhi ya wanaume wamejenga tabia ya kuvumilia matatizo yanayowasumbua kwa
madai kuwa wanakosa muda wa kufika katika vituo vya afya kufanya uchunguzi huku
wengine wakiwa na aibu.
Na Phinna Nimrod Dodoma FM
Comments
Post a Comment