
Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma imewatangazia wananchi wa Dodoma kwamba imeanza zoezi la uuzaji wa viwanja 10,864 ili
kuwapatia fursa na nafasi ya kununua viwanja ndani ya Makao Makuu ya Nchi.
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dododoma GODWIN KUNAMBI amesema mpango huo wa kutangaza ugawaji wa viwanja ni
endelevu na lengo lake ni kumuwezesha kila mwananchi apate fursa ya kununua
kiwanja.
Kunambi amesema
mpango wa Upimaji wa viwanja ulianza mwezi January mwaka 2018 hivyo ni kazi ya
miezi minne na wanatarajia kufikia mwishoni mwa mwezi huu jumla ya viwanja kumi
na tisa elfu mia nne tisini na saba viwe vimeshapimwa.
Amesema maeneo yalinayopimwa
viwanja hivyo ni IYUMBU ambapo vimepimwa viwanja 967, Mtumba viwanja 9897,
Michese 1500 pamoja na Nara viwanja 7000 na tayari viwanja elfu 13 vimekamilika
kwa upimaji.
Zoezi la uuzaji wa
viwanja litafanyika katika Jengo la zamani la halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
kuanzia April 20 mwaka huu ili kuweka
uwazi na uhuru na kila mwananchi anunue kwa haki bila kufanyiwa upendeleo.
Na
Phina Nimrod Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment